Tujivunie, Tukienzi, Tukieneze Kiswahili
Leo hii, tunasherehekea , siku maalum ya kutambua na kuenzi thamani ya lugha ya Kiswahili kama chombo muhimu cha mawasiliano, utambulisho wa tamaduni, na daraja la maelewano baina ya jamii mbalimbali duniani. Lugha, si tu njia ya kuwasiliana, bali ni kielelezo cha fikra, maadili, historia, na matumaini ya jamii. Kiswahili ni lugha ya Kiafrika iliyoenea zaidi barani, na mojawapo ya lugha 10 zinazozungumzwa zaidi duniani, ikiwa na zaidi ya wasemaji milioni 200. Lugha hii inatumika kama lugha ya mawasiliano (lingua franca) katika nchi nyingi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini, na sasa inafundishwa pia katika vyuo vikuu vikuu duniani kote. Ni lugha rasmi ya taasisi kuu za bara letu kama vile (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Kwa kutambua mchango mkubwa wa Kiswahili katika kuimarisha mshikamano, amani, na maendeleo ya Afrika, Julai 7 imetangazwa kuwa Siku ya Kiswahili Duniani. Tarehe hii si ya bahati nasibu, ni kumbukumbu ya siku ya kihistoria mwaka 1954 ambapo Chama cha TANU, chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kilikifanya Kiswahili kuwa lugha ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Viongozi wengine kama Mzee Jomo Kenyatta pia walikitumia Kiswahili kama nyenzo ya kuhamasisha umoja kupitia kaulimbiu ya “Harambee.” Leo, tunapoadhimisha siku hii, tunakumbushwa kwamba lugha yetu ni nguzo ya maendeleo.
Kwa kutambua umuhimu wake duniani kote, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha , likithibitisha zaidi umuhimu wa Kiswahili katika kukuza mshikamano, amani na umoja wa Afrika nzima.
Twajivunia Kiswahili
Kiswahili kilikuwepo, lakini kilipuuzwa. Sasa twajulikana kote ulimwenguni. Hakika tunatamba, hakika twajivunia, Waswahili twaringa kutambuliwa duniani.
Historia Fupi ya Kiswahili
Kiswahili kina historia tajiri na tata iliyochangiwa na tamaduni na lugha mbalimbali kwa karne nyingi. Asili yake imekuwa ikijadiliwa na wataalamu, na kuna nadharia kuu mbili kuhusu namna lilivyoendelea. Nadharia ya kwanza inaeleza kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ambayo ilianza kuibuka katika pwani ya Afrika ya Mashariki kati ya mwaka 100 na 500 BK. Lugha hii ilikua kama lingua franca, yaani lugha ya mawasiliano ya pamoja, iliyosaidia jamii za wasemaji wa Kibantu kuwasiliana na wafanyabiashara kutoka Arabia na Asia. Hatimaye, Kiswahili kilikua kuwa lugha muhimu ya biashara, diplomasia, na mawasiliano ya kitamaduni.
Nadharia ya pili inaangazia ushawishi mkubwa wa lugha ya Kiarabu katika ukuzaji wa Kiswahili. Neno "Swahili" limetokana na neno la Kiarabu 蝉补飞ā?颈濒ī, linalomaanisha "wa pwani", jambo linalodhihirisha uhusiano wa karibu wa kibiashara na kitamaduni kati ya watu wa pwani ya Afrika ya Mashariki na wafanyabiashara Waarabu. Kwa muda, msamiati, sarufi, na hata maandishi ya Kiarabu yaliathiri Kiswahili, hasa katika maeneo ya pwani. Uhusiano huu uliisaidia lugha ya Kiswahili kustawi kama njia muhimu ya mawasiliano, kwa mazungumzo na maandishi, ndani ya Afrika ya Mashariki na hata kimataifa.
"Mwacha mila ni mtumwa"
Mambo ya Kweli kwa Kiswahili
- Ndiyo lugha inayozungumzwa na watu wengi zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na hutumika kama lingua franka katika zaidi ya nchi 14 za Afrika.
- Idara ya Umoja wa Mataifa ya Mawasiliano Ulimwenguni ina operesheni ya .
- Maneno kama vile “Harambee” na “Uhuru” yanaonyesha mizizi mirefu ya Kiswahili katika jamii na umoja.
- Kiswahili awali kiliandikwa kwa maandishi ya Kiarabu kabla ya alfabeti ya Kilatini kuwa sanifu.
- Kiswahili kina muundo wa kimantiki na wa kifonetiki, na kuifanya kuwa miongoni mwa lugha rahisi za Kiafrika kujifunza kwa wanaoanza.
Bidhaa za habari za UN kwa Kiswahili
- Mitandao ya kijamii kwa Kiswahili